CRISTIANO Ronaldo, tayari ameshakamilisha masuala ya vipimo hivyo yupo tayari kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Manchester United na kinachosubiriwa kwa sasa ni utambulisho wake pekee.
United wameeleza kuwa wamefikia makubaliano mazuri na Juventus ambapo alikuwa anacheza mshambuliaji huyo mwenye miaka 36 kwa ajili ya kuipata saini yake.
Masuala binafsi kati ya mchezaji na timu yameshapitishwa na amekubali kusaini dili la miaka miwili kwa sasa dili lake lipo kwenye hatua za mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa usiku wa leo Jumanne ya Agosti 31.
Nyota huyo anakwenda kurejea kwenye Ligi Kuu England anatajwa kuwekewa mkwanja mrefu na atakuwa anapokea pia mshahara mnono kwa wiki jambo ambalo lilimfanya akubali kurejea hapo.
Ronaldo alifunga jumla ya mabao 118 alipokuwa ndani ya Manchester United katika mechi 292 ambazo alicheza kati ya mwaka 2003 na 2009.