Home Yanga SC BAADA YA KAMBI YA YANGA KUYEYUKA, NGUVU IMEELEKEZWA HUKU,SABABU ZATAJWA

BAADA YA KAMBI YA YANGA KUYEYUKA, NGUVU IMEELEKEZWA HUKU,SABABU ZATAJWA

 


KAMBI ya siku 10 ambayo ilipangwa awali kufanyika nchini Morocco kwa timu ya Yanga kukwama kutokana na sababu ambazo zimewekwa wazi kwamba ni maslahi mapana ya timu hiyo pamoja na sababu mbalimbali jambo lililofanya uongozi kuamua kusitisha kambi hiyo sasa ngubu inahamia kwenye wiki ya Mwananchi.

Kilele cha wiki ya Mwananchi kinatarajiwa kuwa Agosti 29, Uwanja wa Mkapa na kwa siku hizo ambazo zimebaki, kambi ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi itakuwa Kigamboni katika kijiji cha Avic Town.

Kambi hiyo ya siku 10 Morocco ilitarajiwa kumeguka rasmi Agosti 27 na kikosi kurejea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Mwananchi pamoja na mechi nyingine ikiwa ni pamoja na ile ya Ngao ya Jamii ila mambo yamekuwa tofauti.

Jana kikosi hicho kilianza safari ya kurudi Dar es Salaam kupitia Dubai na leo kinatarajiwa kutua rasmi kwenye ardhi ya nyumbani.

Taarifa rasmi kutoka Yanga imeeleza kuwa wanarejea Tanzania kwa ajili ya kuendelea na maandalizi pamoja na masuala mengine huku wakiwaomba mashabiki kuendelea kuwa bega kwa bega na timu hiyo.


Pia Yanga wameweka wazi kwamba Agosti 25 ambayo ni kesho itakuwa siku ya uzinduzi rasmi wa uzi mpya wa msimu wa 2021/22 ambao utapatikana katika maduka yote.


SOMA NA HII  YANGA WATOA TAMKO KUTOFUNGA KWA DITRAM NCHIMBI MWAKA MZIMA