Home Yanga SC HIZI HAPA SABABU ZA YANGA KUAMUA KUPELEKA WIKI YA WANANCHI ZANZIBAR

HIZI HAPA SABABU ZA YANGA KUAMUA KUPELEKA WIKI YA WANANCHI ZANZIBAR


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umepanga kuzindua Wiki ya Mwananchi Agosti 22 visiwani Zanzibar ambapo kilele chake kitakuwa Agosti 29, jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari na mawasilano wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa malengo makubwa ni kushirikiana na mashabiki na wapenzi wa timu hiyo huku wakitoa misaada mbalimbali kwa jamii yenye uhitaji maalumu.

“Uzinduzi utafanyika Zanzibar Jumapili hii, hivyo niwaombe mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga,visiwani humo wajiandae kwa tukio hili kubwa ambalo litaambatana na mambo mbalimbali ya kijamii,” amesema.

Aidha Bumbuli amewataka wanachama, mashabiki wa Yanga kukaa tayari kwa ajili ya Wiki ya Mwananchi na kuwahimiza kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

“Tunawaomba wajitokeze kushiriki kikamilifu katika Wiki  ya Mwananchi , lakini pia wajipange kujumuika nasi hapa Dar es Salaam kwa ajili ya kilele Agosti 29 ambapo watapata fursa ya kuona  kikosi chao cha msimu ujao,,” amesema Bumbuli.

Hii ni mara ya pili uzinduzi huo kufanyika visiwani humo ukiambatana na shughuli mbalimbali za kijamii na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Kikosi cha Yanga kwa sasa kiko nchini Morocco kilipoweka kambi kujiandaa na Ligi Kuu Bara na mashindani ya kimataifa.

Baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo ni  Djigui Diarra, Erick Johora, Djuma Shaban, Jesus Muloko, David Bryson, Dickson Ambundo, Khalid Aucho, Heritier Makambo na Fiston Mayele.

SOMA NA HII  GAMONDI AWATAJA MASTAA WAWILI YANGA