Home Uncategorized KAZI IMEANZA SIMBA, NYOTA SABA KUSEPA KIKOSINI MSIMU UJAO

KAZI IMEANZA SIMBA, NYOTA SABA KUSEPA KIKOSINI MSIMU UJAO


INAELEZWA kuwa nyota saba ndani ya Simba safari yao itakuwa imefika tamati kikosini hapo kutokana na sababu mbalimbali msimu wa 2020/21.

Taarifa zinaeleza kuwa mpango mkubwa wa Simba ni kufanya maboresho ndani ya kikosi hicho ili kuleta ushindani kwa msimu wa 2020/21.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa wanawaze kusepa kwa msimu ujao ni hawa hapa:-

Marcel Kaheza anakipiga Polisi Tanzania kwa mkopo mkataba wake unameguka mwishoni mwa msimu na hajaitwa mezani inaelezwa anaweza kuibukia Morocco ambapo kuna timu inahitaji saini yake.

Mohamed Rashid, anakipiga JKT Tanzania kwa mkopo mkataba wake unaisha na mpaka sasa hajui hatma yake.

Shiza Kichuya kiungo ndani ya Simba hajawa na nafasi kikosi cha kwanza tangu aliporejea akitokea nchini Misri.

Tairone Santos raia wa Brazili hajawa chaguo la kwanza mbele ya Sven Vandenbroeck.

Sharaf Shiboub kiungo huyu raia wa Sudan baada ya kurejea kutoka nchini humo ambapo alikwama kutokana na janga la Corona amekuwa adimu kuonekana kikosi cha kwanza.

Hassan Dilunga mkataba wake unameguka na inaelezwa kuwa anahitaji dau la milioni 80 jambo linaloleta mvutano ndani ya timu.

Rashid Juma huyu inaelezwa kuwa atatolewa kwa mkopo kwenda Polisi Tanzania.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema kuwa wataweka wazi hivi karibuni wachezaji ambao wataacha watakapopata ripoti kutoka kwenye benchi la ufundi.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR: TUNABAKI TPL, TABU IPO PALEPALE