Home Yanga SC KISA BAHATI..SHABANI DJUMA AMTAKA MWAMNYETO KUKUNJUA NAFSI..UONGOZI WAFUNGUKA HAYA

KISA BAHATI..SHABANI DJUMA AMTAKA MWAMNYETO KUKUNJUA NAFSI..UONGOZI WAFUNGUKA HAYA


BEKI mwenye uwezo wa kupandisha mashambulizi wa Yanga, Djuma Shabaan amemfuata nahodha wake msaidizi, Bakari Mwamnyeto akimuomba amuachie jezi namba 3. Mkongomani huyo amewaambia wenzie kwamba hiyo ndiyo jezi yake ya bahati na ni spesho kwake ndani ya uwanja.

Mwamnyeto aliitumia msimu uliopita tangu asajiliwe na Yanga akitokea Coastal Union ya Tanga katika usajili ambao ulimfanya kuwa miongoni mwa mabeki ghali nchini.

Akizungumza  kutoka kwenye kambi ya Yanga mjini hapa, Djuma alisema anatamani sana kama Mwamnyeto atakunjua nafsi na kumuachia jezi hiyo ambayo ameitumia kwa muda mrefu akiwa na AS Vita ambapo sasa anataka pia kuitumia akiwa na Yanga lakini hata hivyo bado hajapewa jibu la kukubaliwa.

“Nimemuomba ameniambia tutaongea, kama akikubali nitakuwa na furaha sana, kwangu ni kama namba yenye bahati kubwa, nikifikiria kuikosa naona kama kuna kitu kinapungua, naamini atanikubalia,” alisema. Djuma aliwahi kuwaniwa na Simba, lakini Kocha Didier Gomes akawatolea nje viongozi kulinda kiwango cha Shomari Kapombe.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kwamba hawawezi kuingilia kama Mwamnyeto ataamua kumuachia jezi hiyo Djuma kwa kuwa hayo ni makubaliano yao, ingawa tayari beki huyo Mkongomani ameshapewa jezi nyingine. Mwamnyeto hakufafanua chochote.

“Tulishampa Djuma jezi namba 21 lakini yeye anataka sana namba 3, sasa ni kweli wako katika mazungumzo kama watakubaliana huku kwetu hakuna shida, ni uamuzi wao wawili hakutakuwa na nguvu ya kulazimisha,” alisema Hafidh ambaye ni mmoja kati ya mameneja wakongwe nchini.Beki mpya Mkongomani mwingine, Yannick Bangala kwake hakuna ugumu kwani amepewa jezi namba 4 ambayo msimu uliopita ilikuwa inatumiwa na Said Juma ambaye tayari ameshatua Polisi Tanzania baada ya mkataba wake kumalizika.

Aliyekuwa kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima wakati anaagwa aliomba jezi yake namba 8 apewe mwenzake, Zawadi Mauya, lakini sasa imetua kwa Khalid Aucho, raia wa Uganda.

Winga Jesus Moloko aliyekuwa anaitumia namba 21 akiwa AS Vita ndani ya Yanga atapewa 12 ambayo msimu uliopita haikutumiwa tangu iachwe na nahodha wa zamani wa Yanga, beki Juma Abdul. Kipa wa kigeni Diarra Djigui atabeba jezi namba 39 ambayo imeachwa na kipa Mkenya Farouk Shikhalo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI ZA ROBO FAINAL...SIMBA WAIKIMBIZA YANGA CAF...TAKWIMU HIZI HAPA....