Home news PAMOJA NA KUTOLEWA KWA MKOPO..AME AFUNGUKA HAYA KUHUSU SIMBA..AMTUPIA DONGO GOMES

PAMOJA NA KUTOLEWA KWA MKOPO..AME AFUNGUKA HAYA KUHUSU SIMBA..AMTUPIA DONGO GOMES


LICHA ya kutua Mtibwa Sugar kwa mkopo, beki wa kati wa Simba, Ibrahim Ame, amesema kujiunga kwake na timu hiyo haina maana kwamba hana uwezo, bali hiyo ni fursa kwake kwenda kuonyesha kitu kingine tofauti kabla kurejea katika klabu yake kwa kishindo msimu ujao.

Akizumgumza jana, Ame alisema anapenda kuipa thamani sehemu anayotoka, hivyo kutokana na uwezo aliokuwa nao ndani ya klabu ya Simba anakwenda kuudhihirisha.

“Naamini nitarudi Simba kutokana na uwezo nilionao, katika mechi zote nilizocheza nikiwa na klabu hiyo, naamini ni fundisho kwa watu wengine kwamba unaweza kucheza vizuri lakini bado ukawapisha watu wengine.

“Ninaweza kusema kwamba narudi Simba kwa sababu nitaenda kupata muda sana wa kucheza Mtibwa na nitaonyesha zaidi mimi ni nani na sikuwa Simba kwa kubahatisha tu, ila ni kwa sababu ya uwezo wangu,”alisema Ame.

Kuhusu suala zima la changamoto ya yeye kutolewa kwa kwa mkopo kwenda Mtibwa Sugar, Ame alisema suala hilo halikuwapo kabisa ila ni kwa mipango ya viongozi na yeye pia baada ya kuona hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara akaona ni sawa kwake kuondoka kwa sasa.

“Unajua mnaweza kuwa wanne, lakini nafasi yangu ikawa duni, ila nilipokuwa napata nafasi nilikuwa naonyesha mimi ni Ame, Ame yule yule ambaye mmemzoea kumuona uwanjani akicheza mfululizo. Hiyo nikaona kila siku kukaa nje na uwezo nao unapungua kama mchezaji,” alisema Ame.

Alipoulizwa kuwa haoni kwamba na yeye ni miongoni mwa wachezaji wazawa ambao wanaposajiliwa na timu kubwa huishia kuridhika na mishahara mikubwa pamoja na posho badala ya kuingia katika vita ya kupigania namba na nyota wakigeni na wengine, Ame alijiweka kando kwa kueleza yeye ni mpambanaji ila pengine ni mfumo tu wa kocha umemkataa.

“Hapana mpira siku zote ni kupata nafasi na tukirudi nyuma baada ya mimi kusajiliwa Simba nilikuwa nacheza chini ya Kocha Sven (Vandenbroeck), naamini watu wote waliona Ame ni nani, lakini mambo yakabadilika alipokuja kocha mpya (Didier Gomes) na mipango yake, tukaiheshimu akaamini watu wake, basi ndiyo ikawa hivyo. Hata ukiangalia mechi kama dhidi ya Namungo, Azam na Coastal Union, Ame ni yule Ame kweli,” alisema.

SOMA NA HII  SIMBA WATOA TAARIFA MPYA KUHUSU HALI YA MKUDE...PABLO KUAMUA HATIMA YAKE KIKOSINI...