Home news PANGA LAPITA KAGERA SUGAR, 8 WAACHWA MAZIMA

PANGA LAPITA KAGERA SUGAR, 8 WAACHWA MAZIMA


 UONGOZI wa Kagera Sugar Football Club unapenda kutoa taarifa kwa wanamichezo pamoja na Wanahabari kuwa umeamua kutowaongeza mikataba mipya wachezaji 8 ambao mikataba yao imetamatika mwisho wa msimu wa 2020/2021.

Taarifa rasmi iliyotolewa Agosti 3 na Kagera Sugar ipo namna hii:-

Wachezaji hao wote hawatokuwa sehemu ya kikosi kiatakacho ingia kambini katika maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara 2021/2022 ambayo inatarajia kuanza muda si mrefu.


Wachezaji hao ni Pamoja na:
Benedict Tinocco (mlinda mlango), Haroun Mussa (Beki),Hassan Isihaka (Beki), Ali Sonso(Beki), Mohammed Ibrahim (Kiungo), Mussa Mossi(Kiungo).


 Abdulswamadu Kasim (Kiungo),Vitalis Mayanga(Mshambuliaji).

Makubaliano hayo yamefanyika baina ya benchi la ufundi,wachezaji pamoja na uongozi na kufikia muafaka wa kuwaruhusu waende kutafuta changamoto sehemu nyingine ili waweze kuendeleza mapambano. 

Uongozi unapenda kuwashukuru kwa michango yao mikubwa walioionesha kuipambania timu kwa kujitoa kwa hali na mali tangu siku ya kwanza ambapo waliamua kuwa wanafamilia ya Kagera Sugar hadi leo tunafikia tamati.

Mazuri yenu tutayaenzi na kuyakumbuka daima na hakika mmetuachia maswali magumu sana mioyoni mwetu lakini waswahili wanasema ‘Hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho’.

Tunawatakia kila la Kheri katika changamoto zetu mpya mtakazoenda kukutana nazo katika tasnia hii ya mpira wa Miguu na Mungu awaongoze katika kila hatua mtakayokuwa mnaiendea katika mapambano mapya.
SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZA MSIMU MIKONO MITUPU...HIVI NDIVYO CHAMA 'ANAVYOKICHAFUA' PALE SIMBA SC...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here