Home Yanga SC SIKU CHACHE BAADA YA KUITEMA YANGA..WAZIRI Jr AGOMBANIWA NA TIMU NNE

SIKU CHACHE BAADA YA KUITEMA YANGA..WAZIRI Jr AGOMBANIWA NA TIMU NNE


Baada ya Mshambuliaji Waziri Junior Shentembo kuvunja mkataba na Young Africans, vilabu vinne vya Tanzania Bara vimeripotiwa kumuwania.

Warizi Junior aliutaka Uongozi wa Young Africans kuvunja mkataba wake, ili akatafute changamoto mpya ya kisoka nje ya klabu hiyo kongwe nchini.

Meneja wa Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Toto Africans, Azam FC na Mbao FC Juma Ismail amethibitisha uwepo wa ofa kutoka kwenye vilabu hivyo vinne, ambapo hata hivyo hakutaka kuvitaja hadharani.

“Tumepokea ofa kutoka kwenye vilabu vinne vya Tanzania Bara, tunaendelea kutafakari na siku si nyingi tutaikubali moja ya ofa hizo, “

“Ni mapema kwa sasa kuvitaja hivyo vilabu, lakini tambueni Waziri amepata ofa zaidi ya moja baada ya kuvunja mkataba wake na Young Africans.” amesema Juma.

Hatua ya kuvunja mkataba na Young Africans inamuwezesha Waziri kuwa mchezaji huru, na maamuzi ya kujiunga na klabu yoyote kwa sasa yatakuwa ni maamuzi yake binafsi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWAPOTEZA WAARABU JUZI....GAMONDI AMPANGIA MAJUKUMU HAYA MAPYA PACOME ...