Home Habari za michezo BAADA YA KUZOMEWA NA YANGA JUZI…KICHUYA ‘KWA JEURI’ NAYE KAWAJIBU HIVI KIBABE..

BAADA YA KUZOMEWA NA YANGA JUZI…KICHUYA ‘KWA JEURI’ NAYE KAWAJIBU HIVI KIBABE..

Siza Kichuya wa Namungo na Beki wa Yanga

Kiungo Mshambuliaji wa Namungo FC Shiza Ramadhan Kichuya amesema hajawahi kuchukia wala kushangaa, kuona Mashabiki wa Yanga wakimzomea kila anapocheza dhidi ya timu yao.

Kichuya aliendelea kukutana na kadhia hiyo juzi Jumamosi (Februari 04), wakati wa mchezo wa Mzunguuko wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulimalizika kwa Namungo FC kukubali kufungwa 2-0.

Kichuya ambaye aliwahi kuifunga Yanga katika michezo mitatu tofauti akiwa na Simba SC, amesema kitendo cha kuzomewa na Mashabiki wa Young Afrika anakipokea kama chachu ya kuendelea kupambana na kufanya vizuri anapokuwa uwanjani.

“Mashabiki wa Yanga waendelee kunizomea, tena ninawaomba wanizomee zaidi kwa sababu hiyo kwangu inaniongezea nguvu ya kupambana.”

“Halafu hiyo inanionesha kuwa wanakubali na wanatambua mimi ni mtu gani. Kama wangekuwa hawanizomei maana yake mimi sio lolote.”

“Kwa hiyo waendelee kunizoea, mimi hata sichukii wala siumizwi na hilo.” amesema Kichuya

Tangu alipojiunga na Namungo FC misimu mitatu iliyopita Kichuya hajawahi kuifunga Young Africans, licha ya kupata bahati ya kuwa kwenye kikosi cha klabu hiyo mara zote.

SOMA NA HII  MANULA ATAKA NAFASI YAKE SIMBA, ISHU IKO HIVI