Home Simba SC SIMBA WATIA TIMU MOROCCO KWA AJILI YA KAMBI

SIMBA WATIA TIMU MOROCCO KWA AJILI YA KAMBI


KIKOSI cha Simba kimewasili salama Morocco ambapo kimekwenda huko kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.

Mabingwa hao watetezi walisepa ardhi ya Tanzania jana Agosti 10 na waliweka kambi kwa muda Dubai kabla ya leo kuendelea na safari kuelekea Morocco. 

Wakati wa kuripoti kambini ni Jonas Mkude ambaye alisimamishwa kutokana na utomvu wa nidhamu alikuwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzo kuripoti kambini.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Didier Gomes amesema kuwa maandalizi watakayofanya yatakuwa na matokeo chanya katika msimu ujao.

Pia yupo mfungaji pekee aliyepachika bao ma ushindi katika mchezo wa Kombea Shirikisho kwenye fainali dhidi ya Yanga, Taddeo Lwanga. 

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO ISHU YA MANULA INAVYOIWEKA REHANI SIMBA NA TAIFA STARS....HATIMA YAKE SHAKANI...