Home Yanga SC YANGA WAANIKA MPAGO HUU KUHUSU JEZI MPYA..MASHABIKI KUZIONA NA KUZIVALIA UWANJANI TU

YANGA WAANIKA MPAGO HUU KUHUSU JEZI MPYA..MASHABIKI KUZIONA NA KUZIVALIA UWANJANI TU


UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema sababu kubwa ya kutopanga kutambulisha jezi zao za msimu mpya kwenye uzinduzi wa siku ya Mwananchi, Agosti 22 ni kutokana na kuepuka watu wanaofoji jezi hizo.

Yanga inatarajia kuzindua rasmi siku ya wananchi Zanzibar lakini hawatotambulisha jezi zao mpaka kwenye hitimisho litakalofanyika Agosti 29 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kaimu Katibu mkuu wa Yanga, CPA Haji Mfikirwa amesema jezi tayari zipo tayari lakini watazitambulisha rasmi kwenye hitimisho la siku yao.

“Unajua tukisema tuziweke jezi zetu wazi basi moja kwa moja kuna watu ambao ni kama wapo tayari kwa ajili ya kufungua mitambo yao na kutengeneza feki,” amesema Mfikirwa.

Mfikirwa amesema jezi ambazo zitakuja zitakuwa na viwango vizuri kama vya msimu uliopita na watahakikisha kila mpenzi wa Yanga anaipata.

“Zile ambazo ni mpya wanazitumia kwenye maandalizi ya msimu mpya zipo na zingine pia zipo kwa ajili ya mashindano ambazo ni tofauti na zile,” amesema Mfikirwa.

Mfikirwa ameongeza akisema;”Tunaomba vyombo vya usalama kuwa pamoja nasi katika kuhakikisha tunamaliza suala la uhalifu kwa sababu wanaofoji jezi ni wahalifu.”

SOMA NA HII  KISA TP MAZEMBE...NABI APANGA KUPIGA PANGA LA MAANA KWA MASTAA YANGA...ISHU IKO HIVI..