Home Yanga SC BAADA YA KUAGWA KWA HESHIMA..NIYONZIMA AIBUKA NA HILI KUHUSU YANGA

BAADA YA KUAGWA KWA HESHIMA..NIYONZIMA AIBUKA NA HILI KUHUSU YANGA


LICHA ya kuachana salama na iliyokuwa klabu yake ya Yanga, kiungo fundi wa mpira Mrwanda, Haruna Niyonzima amesema, kwa namna ambavyo Yanga wamesajili watafanya vizuri msimu ujao.

Yanga imemaliza msimu wa 2020/21 ikishika nafasi ya pili, huku ikilitumia vyema dirisha la usajili kwa ajili ya msimu ujao 2021/22 huku pia wakifanya maandalizi makali nchini Morocco.

Kwa mujibu wa Niyonzima, Yanga itakuwa bora zaidi msimu ujao endapo wachezaji watapata muunganiko wa mapema na hasa ikizingatia timu imekuwa mpya kwa asilimia kubwa.

“Usajili wamejitahidi sana japokuwa wengi wao ni wapya ila wakikaa sawa watakuwa bora sana msimu ujao,” anasema Niyonzima.

Anasema kwa namna ambavyo wanajiandaa huko walipo kabla ya ligi kuanza, watafanya makubwa na kuzidisha ushindani hata katika michuano ya Kimataifa ambapo Yanga inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Niyonzima licha ya kuachwa ndani ya kikosi hicho uongozi ulithamini mchango wake na kumuaga kwa heshima kubwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO YANGA YA GSM WALIVYOPINDUA MEZA KIBABE USAJILI WA PHIRI...SIMBA WABAKI WAKILIA...