Home Yanga SC WIKI YA MWANANCHI IMEANZA, YANGA YATOA MAGODORO 30

WIKI YA MWANANCHI IMEANZA, YANGA YATOA MAGODORO 30

IKIWA ni kuelekea katika wiki ya Mwananchi ambapo kilele chake kinatarajiwa kiwa Agosti 29, Uwanja wa Mkapa tayari harakati zimeanza kwa jamii.

Jana Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Klabu ya Yanga, Saady Khimji kwa kushirikiana na viongozi wenzake wa Makao Makuu lakini pia WanaYanga Zanzibar na Serikali walikabidhi magodoro 30 Hospitali ya Mwemberadu Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Mgeni Rasmi wa Shughuli hiyo alikuwa Waziri wa Ardhi na Makazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Juma Pembe.

Ni Khimji aliongoza msafara wa uongozi kutoka makao makuu akiwa ni mwakilishi wa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dr. Mshindo Msolla ambaye alipata dharura iliyomfanya ashindwe kufika katika uzinduzi huo Zanzibar.

Mara baada ya kukabidhi Magodoro hayo Msafara wa Uongozi wa Yanga ulielekea Mkoa wa Kusini Unguja eneo la Ukongoroni kufungua tawi na kuweka jiwe la msingi katika jengo la Yanga lililopo hapo.

Leo shughuli rasmi za uzinduzi zitaanza saa moja asubuhi kwa maandamano kuelekea Kisiwandui na baadae kwenye Mkutano wa Wanachama wote utakaofanyika Ukumbi wa NSSF uliopo eneo la Kariakoo Zanzibar.

SOMA NA HII  VIWANGO VYA CHICO NA NKANE 'VYATIBUA NYONGO' YA NABI...AWAKUMBUKA MOLOKO NA SAIDO..AFUNGUKA HAYA...