Home Yanga SC YANGA WAMEPANIA AISEE..WAPANGA KUSAJILI BEKI WA MILIONI 700, SIMBA WALIMKIMBIA

YANGA WAMEPANIA AISEE..WAPANGA KUSAJILI BEKI WA MILIONI 700, SIMBA WALIMKIMBIA

 


YANGA wamerudi nchini DR Congo na sasa wanataka tena kuchukua beki mwingine na sasa matajiri wa GSM wako katika hatua za mwisho kabisa kumleta beki Yannick Bangala Litombo.

Yanga imeshamalizana kila kitu katika makubaliano na Bangala ambaye wakati wowote wiki hii atawasili nchini kuja kusaini mkataba na klabu hiyo kongwe.

SOMA PIAYANGA KUWEKA KAMBI MOROCCO, SABABU YATAJWA

Bangala sasa anakuja kuchukua nafasi ya Mghana na aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Lamine Moro ambaye amesitishiwa mkataba baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Awali Yanga ilikuwa imlete nchini beki Hennock Inonga ‘Varane rasta’, lakini wakati vigogo wa GSM wakimtumia tiketi ya ndege beki huyo aliwazimia simu kisha kuchukuliwa na Simba.

Bangala aliwahi pia kuhitajiwa na Simba lakini wekundu hao wakachelewa na Waarabu wa FAR Rabbat wakamchukua na sasa anakuja Yanga.

Kumbuka Rabat ndio klabu inayofundishwa na aliyekuwa kocha wa Simba Sven Vandenbroeck ambaye kabla ya kutua hapo alitoka kuwapeleka Simba hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa kisha kesho yake akaacha kazi na kutimkia Morocco.

Tayari Soka la Bongo linafahamu kwamba Bangala ambaye alikuwa katika kikosi cha AS Vita kilichoifunga Simba 5-0 lakini npia msimu huo huo wakitolewa na wekundu hao kutinga hatua ya makundi,ameshaaga kwamba anaondoka huku Yanga jana wakituma barua yake ya kumkaribisha nchini kuja kumalizana na mabosi wa timu hiyo.

Hata hivyo, ili kuipata saini ya beki huyo itawalazimu Yanga kuvunja benki, kwani kwa mujibu wa tovuti ya thamani za wachezaji, Litombo anathamani ya Milioni 700.

SOMA NA HII  DUH!!! HII SASA KALI RAIS YANGA AWAPIGA DONGO SIMBA..."UNATIMUA WACHEZAJI KWA HISIA TU