Simba SC

SIMBA KUTAMBULISHA UZI MPYA LEO

admin September 1, 2021 6:43 am


 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo Septemba Mosi wanatarajia kuzindua uzi mpya kwa ajili ya msimu wa 2021/22.

Ni kazi ya Vunja Bei ambaye ana tenda ya kubuni na kutambulisha uzi mpya wa timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Msimu wa 2020/21 iliweza kuwa na jezi za aina tofauti ikiwa ni pamoja na  iliyokuwa maalumu kwa ajili ya mashindano ya kimataifa na ilikuwa na nembo ya Visit Tanzania. 

Pia walikuwa na uzi maalumu kwa ajili ya Kombe la Shirikisho ambalo walilitwaa kwa kushinda bao 1-0 mbele ya watani zao wa jadi Yanga, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa leo uzi wa mabingwa utajulikana.

AZAM FC WAMPA DILI LA MWAKA MMOJA BEKI MCAMEROON VIDEO:TAZAMA NAMNA BONDIA MNAMIBIA ALIVYOTUA BONGO,KUPAMBANA NA MWAKINYO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply