News

BAADA YA KUACHWA YANGA…NUGAZ AAMUA KUPASUKA YA MOYONI…AWATAJA SENZO NA DK MSHINDO

admin September 2, 2021 8:30 am


Saa chache baada ya kuthibitika hatokuwa sehemu ya Sekretarieti ya Young Africans, aliyekuwa Afisa Muhamasishaji Antonio Nugaz amewaaga Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo.

Nugaz ameondoka Young Africans baada ya mkataba wake wa miaka miwili kufikia kikomo, huku uongozi wa juu wa klabu hiyo ukitangaza kutompa mkataba mpya.

Nugaz ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa: Kwa udhati wa Moyo wangu naomba niwashukuru Kuanzia Uongozi wote wa Yanga chini ya mwenyekiti wetu Dk. Mshindo Mbette Msolla na Kaimu Katibu Mkuu Mpya Senzo Mbatha Mazingiza, wafanyakazi wenzangu wote kwa upendo wenu kwa kipindi chote cha miaka miwili niliyoitumikia @yangasc kwa moyo Mkunjufu na kujitoa kwangu, Mungu awabarik, awalinde na awape kila hitajio la nafsi zenu ili tuweze kuipeleka mbele Brand ya Yanga.

Wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga ninyi mumekuwa na mimi kwa moyo mmoja Ahsanteni sana Nawapenda sana na niatendelea kuwa nanyi.

Tutaonana tena hivi Karibuni. Insha Allah.

HUYU NDIYE DITRAM NCHIMBI HATARI YAKE KILA BAADA YA DAKIKA 243..ACHEZA MECHI NNE TU PAMOJA NA MESSI KUONDOKA …BARCELONA WAKUMBANA NA KISANGA KIPYA KUHUSU JEZI YAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply