news

MAYELE AWATULIZA YANGA, KAZI INAENDELEA

admin September 3, 2021 11:43 am


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kwa kutoa kauli nzito iliyoendana namatarajio ya kuipa mafanikio makubwa timu hiyo.

 

Mayele ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo amesajiliwa akitokea AS Vita ya nchini DR Congo.


Mshambuliaji huyo wikiendi iliyopita kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi, alicheza mechi ya kirafiki dhidi ya
Zanaco iliyomalizika kwa Yanga kufungwa 1-2.


Akizungumza na Spoti Xtra, Mayele alisema: “Mashabiki zetu wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa sasa kwani ndio kwanza tunaanza, timu bado inaandaliwa vizuri na mwalimu, tunaamini kila kitu kitakuwa sawa.


“Sisi kama wachezaji bado tunaendelea kupambana kwa ajili ya kufanya vizuri msimu ujao.

 

Tunataka kuifikisha timu kwenye malengo. Wasubiri waone.“Hakuna ambaye anapenda kuona timu inafanya vibaya, kama ambavyo mashabiki wanaumia pale matokeo yanavyokuwa mabaya basi na sisi wachezaji tunaumia, hivyo hatutakubali hilo litokee.

KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA NA SHIRIKISHO..CAF WASHUSHA RUNGU TZ..WAFUNGIA UWANJA DStv YAZINDUA KIFURUSHI KIPYA KWA GHARAMA NAFUU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply