Home news UZI WA YANGA UNAAMBIWA, ‘SISI TUNA WATU’

UZI WA YANGA UNAAMBIWA, ‘SISI TUNA WATU’


 MABINGWA mara 27 wa Ligi Kuu Bara wanatamba kitaa kwa sasa na uzi wao mpya wa msimu wa 2021/22 ambao ulizinduliwa hivi karibuni Mlimani City.

Mbunifu wa uzi huo ni mzawa Sheria Ngowi huku akiweka wazi kwamba kila nembo iliyotumika katika uzi huo ilizingatia mahitaji ya soko pamoja a uchaguzi wa rangi yenye ubora.

Uzi ambao umeonekana kupendwa na kuuza kwenye maduka ni ule wa rangi ya njano na picha za watu kwa mbali ambazo Ngowi amesema kuwa alizingatia maana halisi ya ‘Sisi Tuna Watu’.

Hata uzi wao ule wenye rangi ya kijani ambao ni uzi wa nyumbani ni miongoni mwenye muonekano pia wa picha hizo za ‘Sisi Tuna Watu’.

SOMA NA HII  AHMED ALLY : MECHI DHIDI YA SIMBA, YANGA WAICHUKULIA KAMA WORLD CUP YAO....