BAADA ya kutangazwa kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingiza amechimba mkwara mzito kuwa ni lazima kikosi hicho kifanye makubwa, na kukamilisha malengo ambayo wamejiwekea ikiwemo kutwaa ubingwa ulio kwa Simba.
Senzo alitangazwa rasmi kushika wadhifa huo ndani ya Yanga kwa lengo la kuhakikisha anakamilisha mchakato wa mabadiliko ya kiuendeshaji kama ambavyo iliazimiwa na Wanachama wa klabu hiyo katika mkutano mkuu uliofanyika Juni 27, mwaka huu.
Kabla ya majukumu hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita tangu amejiunga na Yanga, Senzo alikuwa akihudumu kama mshauri mkuu wa mabadiliko.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Senzo alisema: โTumefanya usajili mzuri katika dirisha la usajili lililopita, lakini tumekuwa na mipango bora kuelekea msimu ujao kama uongozi kuhakikisha tunafikia malengo ambayo tumejiwekea.
โKwangu nikuhakikishie kuwa nina matumaini makubwa ya kukamilisha malengo ambayo tumejiwekea na kurejesha furaha kwa Wanayanga.โ