Uncategorized

MNATA:MUDA MWINGINE UNAPIGA KELELE HUJUI UNAZUGUMZA NINI, PRESHA TUPU

admin April 18, 2020 5:01 pm

METACHA Mnata mlinda mlango namba mbili wa Yanga amesema kuwa ni presha kubwa kuwa ndani ya uwanja kwenye mechi kubwa hasa kwa mlinda mlango mwenye uchungu wa kupata clean sheet.

Mnata amesema kuwa wakati mwingine mlinda mlango anapiga makelele bila kujua anazungumza nini ila sababu kubwa ni presha tu.

“Wakati mwingine ukiwa langoni unazungumza kwa nguvu bila kujua unazungumza nini kutokana na presha ambayo mlinda mlango unakuwa nayo pamoja na yale makelele ya mashabiki.

“Kikubwa ni kuona namna gani unazidi kuwa bora kwenye kazi yako na kushirikiana na wenzako ili kulinda lango kwani kikubwa ni kuona namna gani unamaliza dakika tisini bila kufungwa,” amesema.

Msimu wa 2019/20 Mnata alikaa langoni kwenye dabi yake ya kwanza mbele ya Simba na Yanga ilishinda bao 1-0 Machi 8.

BALOTELI BADO ANA URAFIKI NA NYAVU MBELGIJI WA YANGA KUSHUSHA KIUNGO ATAKAYEMPA CHANGAMOTO TSHISHIMBI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply