hafiz konkani
Habari za michezo

GAMONDI AVUNJA UKIMYA, AFUNGUKA HAYA KUHUSU KONKAN

Staff Desk August 31, 2023 11:32 am

Kocha MKuu wa Yanga raia wa Argentina Miguel Gamondi amesema kuwa hana haraka na straika wake Mghana Hafiz Konkoni kwani anaamini kuwa atampa anachotaka.

Gamondi alisema, anafahamu kuwa mchezaji huyo ni mzuri na ndiyo yupo kwenye klabu hiyo ila kwa sasa anahitaji muda kidogo ili kuweza kuwa bora na kufunga mabao kama ambavyo anatakiwa kufanya.

Miguel Gamondi alisema: “Sina shida na Konkoni, ni mchezaji mzuri ambaye kwa sasa anahitaji muda kuweza kutoa kitu ambacho watu wanahitaji. Najua mashabiki bado hawajapata kitu bora sana kutoka kwake.

“Ili aweze kufika huko anahitaji muda na ndiyo maana nimekuwa nikimpa nafasi yeye pamoja na wenzake wote kwenye kikosi.”

Konkoni amecheza mechi mbili za ligi kuu na kufunga bao moja, lakini bado kumekuwa na mashaka kutoka kwa mashabiki ambao wamekuwa wakitarajia mabao mengi kutoka kwake.

KWA HILI YANGA HII IMESHAKUWA BALAA MSUVA ATOA KAULI NZITO, SIMBA, YANGA ZATAJWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply