KLABU ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imewasilisha majina ya wachezaji 31 waliosajiliwa kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2021/2022.
Klabu hiyo itakayoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imeelezwa kuwa imepeleka idadi kubwa ya wachezaji waliosajiliwa CAF kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo.
Kwa upande wa watani zao Yanga SC, imeelezwa kuwa wao wamewasilisha orodha ya wachezaji 28 waliowasajili kwa ajili ya michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika.
Wachezaji hao waliosajiliwa kwa ajili ya michuano ya Afrika, makipa ni wanne (4) ambao ni; Aishi Salum Manula, Benno David Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salim.
Mabeki ni tisa (9) ambao ni; Erasto Edward Nyoni, nahodha msaidizi Mohammed Hussein Tshabalala, Gadiel Michael, Henock Inonga ‘Varane’, Israel Mwenda, Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma na Shomari Salum Kapombe.
Viungo wapo kumi na tatu (13) ambao ni; Abdulswamad Kassim, Bernard Morrison, Duncan Nyoni, Hassan Dilunga, Jimmyson Mwanuke, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Pape Ousmane Sakho, Peter Banda, Rally Bwalya, Sadio Kanoute, Thadeo Lwanga na Ibrahim Ajibu Migomba.
Washambuliaji wapo watano (5) ambao ni; Nahodha John Raphael Bocco, Meddie Kagere, Chriss Mugalu, Yusuph Mhilu na Kibu Denis.