news

POLISI TANZANIA WAJICHIMBIA KANDA YA ZIWA

admin September 7, 2021 10:43 am


 KIKOSI cha Polisi Tanzania chimbo lao kwa sasa kwa ajili ya msimu wa 2021/22 ni pale Mwanza, Kanda ya Ziwa.

Uwanja unaotumika kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao ni ule wa CCM Kirumba ilipo ngome yao ni pale Moshi na huwa wanatumia Uwanja wa Ushirika.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri.

“Tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa 2021/22 na kila kitu kinakwenda sawa hivyo imani yetu ni kuweza kufanya vizuri kwa msimu ujao ili kupata matokeo chanya.

“Kwa usajili ambao tumefanya na namna ambavyo tunazidi kujiandaa tuna amini tutafanya kazi nzuri, mashabiki wawe pamoja nasi,” amesema.

Miongoni mwa nyota wapya ambao wamesajiliwa ni pamoja na kipa Metacha Mnata aliyekuwa akiitumikia Yanga, Tariq Simba aliyekuwa akiwatumikia Biashara United ya Mara.

MWANZILISHI WA SIMBA DAY ATIA HURUMA..ANAISHI KWA MATESO…AMTAJA MO DEWJI..SIMBA WATOA TAMKO… HAJI MANARA AKARIBISHWA NA WAZEE WA YANGA, ATAJA DENI KWA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply