RAIA wa Misri, Mohamed Salah anaingia kwenye rekodi ya washambuliaji walioweza kufikisha jumla ya mabao 100 ndani ya Ligi Kuu England ambayo inatajwa kuwa namba moja kwa kupendwa na kufuatiliwa duniani.
Mshambuliaji huyo anayekipiga ndani ya Liverpool inayonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp aliweza kufikisha jumla ya mabao 100 baada ya kutupia bao moja kwenye mchezo wa Ligi Kuu Engand dhidi ya Leeds United.
Ilikuwa ni Septemba 12 nyota huyo aliweza kuandika rekodi hiyo ambayo ni mpya kwake wakati timu yake iliposhinda kwa mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao Leeds United, Uwanja wa Elland Road.
Alipofikisha mabao 100 wengine ambao waliweza kutupia kwenye mchezo huo ni Sadio Mane raia wa Senegal alitupia dakika ya 90 na Fabinho huyu alitupia dakika ya 50 zikiwa zimepita dakika 30 kutoka nyota huyo kufunga bao la kuongoza dakika ya 20.
Anakuwa ni mchezaji wa 30 kuweza kufikisha jumla ya mabao 100 ndani ya Ligi Kuu England na ni mchezaji wa pili kwa wachezaji wanaotoka Afrika kuweza kufikisha idadi hiyo.
Awali rekodi hiyo ilikuwa miguuni mwa Didier Droba, mwili jumba mtu wa kazi ambaye alikuwa amefikisha jumla ya mabao 104.
Anaingia kwenye rekodi za wachezaji ambao wamefunga mabao 100 kwa haraka zaidi ambapo katika orodha hiyo kinara ni Alan Sheare yeye alifunga mabao 100 baada ya kucheza jumla ya mechi 124.
Harry Kane yeye baada ya kucheza mechi 141,Sergio Arguero ilikuwa ni baada ya kucheza mechi 147, Thierry Henry baada ya mechi 160 na yeye Salah amefikisha mabao 100 baada ya kucheza jumla ya mechi 162.
Ikumbukwe kwamba nyota huyo alitua ndani ya kikosi hicho mwaka 2017 akitokea ndani ya AS Roma ni chaguo namba moja la Klopp.