news

MWAKALEBELA ; HATUKUJIANDAA VIZURI…. KAMBI YA MOROCCO NI KAMA HAIKUWEPO TU

admin September 14, 2021 1:00 am

 


Uongozi wa Yanga umekiri timu yao haikuwa na maandalizi mazuri ya msimu mpya.

Uongozi umebainisha hayo baada ya Yanga kuruhusu kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Rivers United ya Nigeria kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wanajipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano Septemba 19 nchini Nigeria.

“Leo tumepoteza mechi ya nyumbani, tunakiri maandalizi yetu ya pre season hayakuwa mazuri, ni kama hayakuepo ila tunajipanga,” amesema.

Kocha Nabi aliwahi kubainisha kuwa hajapata muda wa kutosha kwenye maandalizi ya timu yake iliporejea nchini ikitokea Morocco ilipoweka kambi ya muda mfupi ikiwa ni siku kadhaa kabla ya mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Zanaco ambayo pia Yanga ilipoteza kwenye uwanja wa Mkapa.

SIMBA YAIGOMEA NAMUNGO, KAZI INAENDELEA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply