KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnars Solskjaer amesema kuwa mchezaji wake Cristiano Ronaldo alipaswa apewe penalti mbili kwenye mchezo wao wa jana wa Ligi Kuu England dhidi ya West Ham United.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa baada ya dakika 90, Uwanja wa London ulisoma West Ham United 1-2 Manchester United na mabao yalifungwa na Said Benrahma dakika ya 30 kwa West Ham na liliwekwa usawa na Ronaldo dakika ya 35 na kuwafanya waende mapumziko wakiwa wametoshana nguvu.
Bao la ushindi kwa United lilifungwa na Jesse Lingard dakika ya 89 na kuwafanya United kusepa na pointi tatu mazima huku kipa wao David de Gea akiwa ni nyota wa mchezo kwa kuwa aliweza kuokoa penalti ikiwa ni mara ya kwanza kwake tangu mwaka 2014 alipofanya hivyo walipocheza na Everton.
Solskjaer amesema kuwa ni kiwango kikubwa ambacho kimeonyeshwa na de Gea kwa kuokoa penalti huku akiamini kwamba mchezaji wake Ronaldo alipaswa kupewa penalti mbili moja kipindi cha kwanza na nyingine kipindi cha pili.
“Ulikuwa ni mchezo mzuri wa kukimbizana, shukrani kwa wachezaji namna ambavyo wamefanya, de Gea ameweza kutupa pointi mbili muhimu lakini ninaona kwamba kuna penalti ambazo ilibidi apewe Cristiano kipindi cha kwanza na cha pili,” .