news

YANGA WAREJEA TANZANIA SALAMA KUTOKA NIGERIA

admin September 20, 2021 6:43 am


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Septemba 20 kimewasili salama katika ardhi ya Tanzania kikitokea nchini Nigeria.

Mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara walikuwa wakipambana kwa ajili ya kupeperusha bendera kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Deni lao kubwa ilikuwa ni kwenye kupindua meza kibabe mbele ya Rivers United kwa sababu katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United hivyo walitakiwa kushinda mabao zaidi ya mawili.

Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Rivers United pia jana na mchezo ulipokamilika walianza safari kurudi Tanzania. 

Ni Shirika la Ndege la Tanzania walitumia ndege bora na wameweza kurudi salama Tanzania leo Septemba 20.


MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU SIMBA YAWASHURKURU MASHABIKI, UZEMBE WA SAFU YA ULIZI WAIPA MAUMIVU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply