IKIWA Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza kwa msimu mpya wa 2021/22 na pazia linatarajiwa kufunguliwa Septemba 25 kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba v Yanga, Uwanja wa Mkapa, uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa kufikiria kutwaa mataji ni kujitesa.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit ambaye amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwa Waandishi wa Habari pamoja na kuwa na rekodi za kutosha ameweka wazi kuwa tangu Azam FC itwae taji mara moja msimu wa 2013/14 haijatwaa tena hivyo hesabu kubwa zipo katika kufanya vizuri zaidi msimu mpya.
Mechi yao ya ufunguzi inatarajiwa kuchezwa Septemba 27 itakuwa dhidi ya Coastal Union, Tanga Mkwakwani. Zakazi amesema kuwa kujiwekea malengo ya kutwaa mataji ni kujitesa. Kuhusu kinachoamua matokeo kwenye mechi za Dabi ambazo ni dhidi ya Simba, Yanga na KMC Zakazi amesema kuwa ni vitu vidogo vinavyoamua matokeo.