news

REDONDO NYOTA YAKE YAWAKA

admin September 21, 2021 12:43 pm


 KIUNGO wa Biashara United, Ramadhan Chombo (Redondo), Jumamosi iliyopita alionyesha kiwango cha juu baada ya kufunga mabao mawili wakati timu yake ya Biashara ilipowachapa FC Dikhil ya Djibout mabao 2-0.

 

Mbali na kufunga mabao hayo, kiungo huyo wa zamani wa Simba ameingia kwenye kitabu cha kuwa mchezaji wa kwanza wa Biashara United kufunga mabao mawili na kukosa penalti kwenye mchezo mmoja wa kimataifa.

 

Redondo ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba alionyesha kiwango hicho kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi FC Dikhil ya Djibout na kwenda hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 3-0.


Hii ni mara ya kwanza kwa Biashara United kushiriki mashindano ya kimataifa na imeanza kufanya vizuri kuipeperusha bendera ya Tanzania.


Pia hata Azam FC ya Tanzania nayo imeweza kusonga mbele katika hatua ya awali na kutinga raundi ya kwanza.

MAPICHAPIPICHA SIMBA WAKISAINI DILI JIPYA NEEMA ZAZIDI KUSHUKA SIMBA…BAADA YA ATCL KUMWAGA MAMILIONI..LEO WASAINI DILI LINGINE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply