CRISTIANO Ronaldo, staa wa Klabu ya Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer amekiri kuwa Ligi Kuu England ni ngumu zaidi kutokana na kuwa na kazi ngumu katika mechi ambazo wanacheza.
Septemba 19, Manchester United iliweza kupata ushindi kwa mbinde mbele ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa London jambo lililomfanya staa huyo akiri wazi kuwa muziki wanaokutana nao sio wa kitoto.
Katika mchezo huo Ronaldo alipachika bao dakika ya 35 na lile la ushindi lilipachikwa dakika ya 89 na Jesse Lingard huku bao pekee la West Ham lilipachikwa dakika ya 30 na Said Benrahma. Pia kipa wa Manchester United alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kuwa aliweza kuokoa penalti.
Ronaldo anacheza Premier League msimu huu baada ya kusepa huko miaka 12 iliyopita alicheza La Liga ndani ya Real Madrid pia ameibuka United akitokea Juventus inayoshiriki Serie A ambapo awali dili lake lilikuwa linatajwa kukamilika ndani ya Manchester City kabla ya simu moja ya mabosi wa United kuvuruga mipango.
Nyota huyo amesema:”Kila mechi ya Premier League ni lazima upambane kupata pointi tatu, hii inaonyesha ligi ni ngumu,”.
Pia leo Manchester United ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya West Ham United katika Uwanja wa Old Trafford ila utakuwa ni mchezo wa Carabao.