YANGA itakipiga dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Jumamosi Septemba 25 na kwenye kikosi chao watamkosa kiungo wao wa nguvu, Mukoko Tomombe.
Mukoko atakosekana kwenye mchezo huo kutokana na adhabu ya kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyoonyeshwa kwa kosa la kumpiga kiwiko mshambuliaji wa Simba, John Bocco.
Kiungo huyo alionyeshwa kadi hiyo kwenye mchezo wa fainali Kombe la Azam uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma na Simba kufanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kushinda bao 1-0.
Kukosekana kwa Mukoko ambaye ni kiungo mkabaji na mzoefu kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara, kunamfungulia milango Aucho ambaye tangu amejiunga na timu hiyo hajacheza mchezo hata mmoja kutokana na ITC yake kuchelewa na mashabiki wataanza kuuona mziki wa nyota huyo kwenye mchezo huo wa Septemba 25.