news

OMOG AKABIDHIWA MIKOBA YA HITIMANA ALIYEIBUKIA SIMBA

admin September 23, 2021 5:43 am


JOSEPH Omong amekabidhiwa mikoba ya Thiery Hitimana ambaye alipaswa kuwa ndani ya Mtibwa Sugar ya Morogoro na sasa yupo zake Simba.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa tayari kocha huyo amepewa majukumu kuinoa Mtibwa Sugar.

Awali majukumu ya kuinoa Mtibwa Sugar ilibidi yawe mikononi mwa Hitimana ambaye aliletwa Tanzania na timu ya Mtibwa Sugar ila kabla ya kuwaga wino kuinoa timu hiyo mabosi wa Simba wakamvutia kasi na sasa ameshaanza kazi kwenye kikosi hicho.

Kifaru amesema kuwa ni maombi zaidi ya makocha 72 walikuwa nayo mkononi ila wao waliweza kufanya mchujo wao na kufika makocha watano na hatimaye sasa ni Omog atakuwa mbeba mikoba iliyoachwa wazi na Hitimana.

Raia huyo wa Cameroon amewahi kuifundisha Azam FC, AC Leopards pia na Simba hivyo ana uzoefu mkubwa na soka la Tanzania.


NYOTA SABA KIKOSI CHA KWANZA KUUZWA NA MANCHESTER UNITED JAMES RODRIGUEZ KUIBUKIA AL RAYYAN

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply