BEKI wa Barcelona, Gerard Pique ametaka utulivu kikosini hapo kufuatia timu hiyo kuyeyusha pointi mbili katika Ligi ya Ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania, (La Liga).
Pique amesema kuwa Barcelona inasumbuliwa na tatizo la mabadiliko ambayo yametokea kwa muda huu ila anaamini kwamba yatapita.
Hayo yamekuja baada ya timu hiyo kulazimisha suluhu dhidi ya Cadiz huku presha kubwa ikiwa kwa Kocha Mkuu, Ronald Koeman ambaye timu yake imeshinda mechi mbili tu kati ya tano ilizocheza msimu huu.
“Tulikuwa na mabadiliko ya rais na makocha hivi karibuni na tunahitaji kwa sasa umoja pekee. Sote tunatakiwa kujiweka katika njia moja. Haitakuwa na msaada kama timu haitakuwa na umoja,” .