Home news BAADA YA NGAO YA JAMII NGUVU YA YANGA IPO HUKU

BAADA YA NGAO YA JAMII NGUVU YA YANGA IPO HUKU


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa baada ya kumaliza kazi yao ya kusepa na taji la Ngao ya Jamii mbele ya Simba kwa ushindi wa bao 1-0 sasa nguvu zao ni kwenye Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Makao Makuu ya Yanga, Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanashukuru uwepo wa mashabiki pamoja na kazi kubwa iliyofanywa na benchi la ufundi linaloongozwa na Nasreddine Nabi.

“Tunashukuru kwa kuwa tumeweza kutwaa Ngao ya Jamii ni kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi na tumeanza awali kabisa kufanya hivyo maana yake ni kwamba kuna kazi kubwa ambayo tutaifanya.

“Shukrani kubwa kwa mashabiki, kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi na kutupa ushirikiano, kuna raha kubwa kwa kushinda taji tena kuwafunga watani wa jadi.

“Sherehe za ubingwa kwa sasa zimekwisha na nguvu inakwenda kwenye mechi za Ligi Kuu Bara, tunakwenda kuanza kazi mbele ya Kagera Sugar hakuna namna ni wapinzani wazuri tunawaheshimu na wana kocha mwenye mbinu ambaye ni Francis Baraza.

“Kikosi kimeondoka leo na wachezaji 25 pamoja na benchi la ufundi, sisi tutakwenda kesho kuungana na timu, kikubwa ni kuendelea kuonyesha ushirikiano kwani kazi ni ngumu na ushindani utakuwa mgumu,” amesema.

Tayari kikosi cha Yanga kimefika salama Kagera tayari kwa maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 29, Uwanja wa Kaitaba.


SOMA NA HII  YANGA YA GSM WEKA MBALI NA WATOTO..KUANZIA MSIMU UJOA USAJILI WOTE KUFANYWA KIULAYA ULAYA...