Home news KIKOSI CHA SIMBA KUIFUATA DODOMA JIJI KWA MTINDO HUU

KIKOSI CHA SIMBA KUIFUATA DODOMA JIJI KWA MTINDO HUU


KIKOSI cha Simba leo kimeanza safari kuelekea Dodoma ambapo kitapita Dar es Salaam kabla ya kuunganisha safari yao na kuibukia Dodoma.

Simba ilikuwa Mara ambapo jana Septemba 28 kilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United. 

Katika mchezo huo Simba iligawana pointi mojamoja na Biashara United baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Karume kusoma Biashara United 0-0.

Inajiandaa na mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya  Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Itakuwa ni Oktoba Mosi na timu zote zinapambana kusaka pointi tatu katika mchezo huo wa ligi.

SOMA NA HII  SAKHO AFICHUA TABIA ZA SARR NNJE YA UWANJA ...ATAJA USTARABU, DHARAU NA KUJIONA....