News

YANGA NGUVU ZAO KWA GEITA GOLD

admin September 30, 2021 10:43 am


CEDRIC Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa nguvu kwa timu hiyo zinaelekea katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa,  Oktoba 2.

Jana Septemba 29, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba na mtupiaji wa bao alikuwa ni Feisal Salum aliyemtungua kipa wa Kagera Sugar,  Chalamanda.

Kaze amesema wataendelea kukijenga kikosi na timu itazidi kuimarika sasa wakielekeza nguvu zao katika mchezo unaofuata

“Mechi ya kwanza ya ligi, ushindi ugenini, tunaendelea kujenga timu na tutaimarika zaidi. Mechi inayofuata inakuja  siku 3 mbele, dhidi ya Geita Gold, tuko nyumbani,”.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije mchezo wake wa kwanz ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Namungo.

UFALME WA TSHABALALA NA KAPOMBE WATIKISWA MWAMNYETO:KAZE ATAONGEZA JAMBO NDANI YA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply