Home kimataifa ARSENAL SHANGWE YAREJEA KITAA, GABRIEL AFANYA KAZI CHAFU

ARSENAL SHANGWE YAREJEA KITAA, GABRIEL AFANYA KAZI CHAFU


SHANGWE limeanza kurejea ndani ya mioyo ya mashabiki wa Arsenal baada ya timu yao kuambulia ushindi wa kwanza ndani ya Ligi Kuu England kwa msimu wa 2021/22.

Bao pekee la ushindi lilioachikwa na nahodha Pierre Aubameyang dakika ya 66 na kufanya ubao wa Uwanja wa Emirates kusoma Arsenal 1-0 Norwich City. 

Arsenal walikuwa wamecheza jumla ya mechi tatu na walikuwa bado hawajapata ushindi ndani ya uwanja jambo ambalo lilikuwa linampasua kichwa Kocha Mkuu, Mikel Arteta. 


Katika mchezo huo Arsenal walipiga jumla ya mashuti 30 huku 7 pekee yakilenga lango na wapinzani wao Norwich City walipga jumla ya mashuti 10 na ni shuti moja lililenga lango.

Nyota wa mchezo ni Gabriel Magalhaes ambaye aliweza kutimiza majukumu yake kwa ukamilifu kwa nafasi yake ya ulizi alionekana akifanya kazi zile wanazoita chafu

SOMA NA HII  YANGA KUMLETA CHID BENZ VS MADEAMA