Home kimataifa ARTETA TAMBO KIBAO HUKO

ARTETA TAMBO KIBAO HUKO


MIKEL Arteta,  Kocha Mkuu wa Arsenal amewapigia saluti vijana wake jambo ambalo linamfanya ajivunie kuwa nao kutokana na kazi kubwa wanayoifanya baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu England. 

Bao pekee la ushindi katika mchezo huo lilipachikwa na Martin Odegaard kipindi cha kwanza ilikuwa dakika ya 30 kwa pigo huru lililozama mazima ndani ya nyavu za wapinzani wao.

Mpaka dakika 90 zinakamilika Uwanja wa Turf Moor, Arsenal walipiga jumla ya mashuti 13 na ni matatu pekee yalilenga lango huku wapinzani wao Burnley waliokuwa nyumbani walipiga jumla ya mashuti 18 na ni mashuti matatu yalilenga lango.

Sasa Arsenal inafikisha jumla ya pointi sita ikiwa nafasi ya 13 huku Burnley ikiwa nafasi ya 19 na pointi yake moja na zote zimecheza jumla ya mechi tano huku kinara akiwa ni Liverpool kibindoni ana pointi 13 anafuatiwa na mabingwa watetezi Manchester City wenye pointi 10.

SOMA NA HII  SHAFFIH DAUDA AZIDI KUTIA 'KUTIA NDIMU' SAKATA LA SIMBA KUKATAA KUVAA NEMBO YA GSM..ADAI NI MSIBA...