Home news DODOMA JIJI KAZI INAENDELEA, WARYDI RASMI MAKAZI YAO MAKAO MAKUU

DODOMA JIJI KAZI INAENDELEA, WARYDI RASMI MAKAZI YAO MAKAO MAKUU


UONGOZI wa Dodoma Jiji umeweka wazi kuwa kwa sasa unaendelea na  maandalizi yake makao makuu ya Tanzania, Dodoma baada ya kumaliza kambi waliyoiweka pale Morogoro.

Timu hiyo ipo chini ya Kocha Mkuu, Mbwana Makata ambaye alikipandisha kikosi hicho kutoka Ligi Daraja la Kwanza ambayo kwa sasa inaitwa Championship.

Msimu wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa 2020/21 aliweza kukiongoza kikosi hicho kumaliza kikiwa nafasi ya nane na pointi zao 44.

Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya na watapambana kufanya vizuri.

“Tuliweka kambi Morogoro ila kwa sasa tumesharejea Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mechi zetu za ligi na kila kitu kinakwenda sawa.

‘Tunaamini kwamba utakuwa ni msimu mgumu lakini hakuna namna maandalizi mazuri na kila mmoja kuhitaji kupata matokeo kutatupa nguvu wakati ujao kikubwa mashabiki kuwa nasi kila wakati,” amesema.

Kwenye ligi mchezo wao wa ufunguzi unatarajiwa kuwa Septemba 28 itakuwa dhidi ya Ruvu Shooting,Uwanja wa Jamhuri.


SOMA NA HII  HABARI YA MANARA KUTOKA SIMBA NA KUTUA YANGA YAWA GUMZO MISRI...WAANDISHI WAHOJI