Home Makala JEMBE:MPIRA WA TANZANIA UNAPASWA KUPEWA THAMANI

JEMBE:MPIRA WA TANZANIA UNAPASWA KUPEWA THAMANI


MWANDISHI mkongwe kwenye masuala ya Habari za Michezo, Tanzania mwenye rekodi za kufanya kazi mbalimbali kubwa ndani na nje ya Tanzania, Saleh Jembe amesema kuwa kuna haja ya kuupa thamani mpira wa Tanzania kwa kuanzia na suala la viingilio.

Maneno hayo amaeyazungumza kwenye kipindi cha Krosi Dongo ambacho kinarushwa ndani ya 255 Global Radio pamoja na Global TV Online.

Jembe amesema:”Ikiwa sehemu kuna msanii anatumbuiza labda ni Kiba, (Alikiba) au Diamond kiingilio ni shilingi elfu ishirini ama elfu 50 watu wanakwenda.

“Lakini unakwenda kuwaona wachezaji kama akina Morrison,(Bernard) Banda, (Peter) Makambo,(Heritier) Aucho,(Khalid) Djuma na burudani ya uwanjani unaijua jinsi ilivyo ni raha kuna vitu vingi.

“Unakutana na watu tofauti lakini shilingi elfu 10 unaona kama unaonewa, si kweli sisemei hii mifano unaweza kukataa hapana, nimepata bahati ya kwenda Ulaya nimeona namna jinsi ilivyo huko.

“Tiketi ya kiwango cha chini nililipia shilingi laki moja na ishirini na tano na mara ya mwisho niliwahi kulipa tiketi kwa shilingi laki tatu na themanini ya Tanzania achana na gharama ya tiketi ya ndege.

“Sio kwamba mimi ni tajiri hapana ni ile furaha yangu ya kwenye mpira, nakumbuka namna nilivyokuwa Uwanja wa Anfield watu wanaimba najiskia raha nimetumia fedha lakini ile furaha bado nipo nayo.

“Tunapaswa kuupa thamani mpira wetu, thamani yake ni kubwa tena kwa mechi za Simba v Yanga hii ni lazima iwe ya thamani. Kuna marafiki wengi wakubwa kutoka nje walikuwa wanakuja kuutazama mchezo hivyo kuna haja ya kuipa thamani,” amesema.

SOMA NA HII  OSCAR OSCAR: NINA IMANI NA MASHAKA JUU YA KOCHA MPYA SIMBA..UWEZO WAKE UMEPOROMOKA...