Home news KAIMU OFISA HABARI SIMBA KUONDOKA

KAIMU OFISA HABARI SIMBA KUONDOKA


 EZEKIEL Kamwaga, Kaimu Ofisa Habari wa Klabu ya Simba amesema klabu hiyo inaendelea na mchakato wa kumtafuta Ofisa Habari kwani yeye ataondoka hivi karibuni kwenda nchini Uingereza.

Kamwaga alipewa nafasi hiyo kwa muda wa miezi miwili baada ya aliyekuwa kwenye nafasi hiyo Haji Manara kubwaga manyanga.

Wakati huu Manara yupo zake ndani ya Yanga akiwa kwenye kitengo cha Ofisa Habari.

Kamwaga amesema:-“Ninakaimu nafasi ya Ofisa Habari kwa muda wa miezi miwili, mwezi ujao nitakuwa naondoka Simba naenda UK, hivyo klabu itamtangaza Ofisa Habari mpya. Mchakato unaelekea kukamilika.
  
“Simba ni ile ile, mashabiki ni wale wale niliowaacha 2013, kilichobadilika sana Simba, imeanza kuwa klabu yenye watu wenye heshima zao, sasa hivi kuna watu kama akina Dr Janabi, akina Mo Dewji, Barbara. Lakini pia sasa kuna mabadiliko kwenye social media,” .
 
 


SOMA NA HII  SIMBA SC "MECHI NA HOROYA NI USHINDI TU"...HUU HAPA UNDANI WA MAANDALIZI ...KIBU YUPO FIT