Home Simba SC HASSAN DALALI AITAKA REKODI YA 2007 MBELE YA YANGA

HASSAN DALALI AITAKA REKODI YA 2007 MBELE YA YANGA


 HASSAN Dalali, aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba amesema kuwa wazee wa timu hiyo wamekubaliana kwamba washinde mchezo wao wa ligi dhidi ya Yanga ili kuirudia rekodi ya 2007.


Julai 3, Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuchezwa mchezo wa kukata na shoka kati ya Simba na Yanga baada ya ule wa awali ambao ulipangwa kuchezwa Mei 8 kuyeyuka kutokana na mabadiliko ya muda jambo ambalo liligomewa na Yanga kwa kueleza kuwa ni kinyume cha kanuni.


Akizungumza na Spoti Xtra, Dalali alisema kuwa mchezo dhidi ya Yanga huwa unakuwa na presha kubwa jambo ambalo huwafanya wengi washindwe kutulia ila anakiamini kikosi cha Simba kitashinda na kutwaa ubingwa kama 2007.


“2007 Morogoro tulicheza Uwanja wa Jamhuri dhidi ya Yanga na tuliwafunga na kuchukua ubingwa katika fainali hiyo ambayo ilikuwa ngumu na mimi nilikuwa ni mwenyekiti.


“Kuna raha sana kuwafunga na kuchukua ubingwa miguuni mwa Yanga hivyo nina amini kwamba linakwenda kutokea licha ya kwamba utakuwa ni mchezo mgumu kwa pande zote mbili.


“Wakati ule ligi ilikuwa inachezwa kwa vituo na timu zilikuwa chache, ukishindwa unashuka daraja na ulikuwa mchezo wa fainali tulishinda kwa panalti baada ya kutoshana nguvu katika muda wa awali,” alisema Dalali.


Kwenye mchezo huo uliochezwa Julai 8,2007 rekodi zinaonyesha kwamba dk 90 zilikamilika kwa timu kufungana bao 1-1 na kwenye changamoto penalti Simba ilishinda penalti 5-4.


Ikiwa Simba itashinda mchezo wake wa Julai 3, Uwanja wa Mkapa itatangazwa kuwa bingwa wa ligi kwa kuwa pointi 76 ambazo atafikisha hazitafikiwa na watani zao Yanga walio na pointi 67 pamoja na Azam FC wenye pointi 64.

SOMA NA HII  KWENYE HILI SIMBA MI BORA KULIKO YANGA