Home Azam FC FEI TOTO AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA HALI YAKE AZAM

FEI TOTO AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA HALI YAKE AZAM

Habari za Azam FC

Kiungo Mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema anainjoi kuichezea timu hiyo, lakini akikiri kuna ushindani zaidi kwa msimu huu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Nyota huyo aliyewahi kukipiga Young Africans, juzi Alhamis (Septemba 21) alienguliwa kwenye kilele cha wafungaji wa ligi baada ya Jean Baleke wa Simba SC kufunga hat trick dhidi ya Coastal Union na kufikisha mabao matano.

Fei Toto amesema, anayo furaha kuwepo Azam FC, kwa sasa anaamini uwepo wake utaisaidia timu kwa kushirikiana na wenzake kufanya vizuri, lakini akisema ushindani kwa msimu huu ni mkubwa kuanzia kwa timu shiriki hadi wachezaji wenyewe kwa wenyewe kitu kinachosaidia kukuza soka la Tanzania.

Nyota huyo wa zamani wa JKU, amesema; “Naenjoi sana hapa nilipo kwa sasa naamini wakati wa Mungu ndio umenifikisha hapa cha muhimu kupambana kufikia malengo.”

Katika hatua nyingine Fei amempongeza Baleke kwa kuwa mchezaji wa pili kupiga hat trick katika Ligi Kuu baada ya yeye kutangulia wakati Azam ikiifumua Tabora United kwa mabao 4-0.

“Nimefurahi kuona mchezaji mwingine anafunga hat trick ni jambo jema na zuri sana napenda na wengine wafunge pia ili tuweke historia itakayozidi misimu mingine” alisema.

SOMA NA HII  KISA MWANAYE KUSAINI YANGA...BABA'KE SURE BOY ASHINDWA KUJIZUIA..ADAI SIO SHABIKI WA YANGA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here