Home Habari za michezo IBRAHIM BACCA ACHUKUA MAAMUZI MAGUMU YANGA, AJIPIGA KITANZI KIREFU

IBRAHIM BACCA ACHUKUA MAAMUZI MAGUMU YANGA, AJIPIGA KITANZI KIREFU

Habari za Yanga

BEKI wa kati, Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ ameongeza mkataba wa kuendelea na kazi katika klabu ya Yanga hadi mwaka 2027.

Bacca (26) aliyejiunga na Yanga Januari 14, mwaka jana akitokea KMKM ya Zanzibar anapewa mkataba mpya baada ya kazi nzuri aliyofanya mwaka mmoja akiwa timu ya Wananchi.

Sambamba na kumuongeza mkataba, Yanga imempa heshima Bacca kwa kuifanya mechi yake ya pili ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam iwe siku maalum ya mlinzi huyo hodari, yaani ‘Bacca Day’.

Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) kila moja zimdhamini Bacca Day kwa dau la Sh. Milioni 20, maana yake Yanga imetengeneza Sh. Milioni 40 tukio maalum la mchezaji huyo.

Ikumbukwe Yanga ilianza mechi zake za Kundi D kwa kuchapwa 3-0 na wenyeji, CR Belouizdad Ijumaa Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria, huku Al Ahly wakiichapa Medeama ya Ghana 3-0 Uwanja wa Al Salam Jijini Cairo.

SOMA NA HII  SIMBA BADO KUNAFUKUTA MOTO...ZIMBWE JR AWAACHIA MSALA HUU WAZAWA