Home news KAZE KUIBUKIA YANGA,KUANZA KAZI MBELE YA SIMBA

KAZE KUIBUKIA YANGA,KUANZA KAZI MBELE YA SIMBA

 CEDRIC Kaze aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2020/21 kabla ya kuchimbishwa lwa kile kilichoelezwa kuwa mwendo mbovu wa timu na kutokwenda sawa na falsafa ya timu hiyo ametua Bongo usiku wa kuamkia leo.



Inaelezwa kuwa ametua kwa ajili ya kumalizana na mabosi wake wa zamani Yanga ambao wanahitaji huduma yake.

Anatarajiwa kuwa kwenye benchi la ufundi akiwa ni kocha msaidizi akishirikiana na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.

Kabla ya kusepa baada ya kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic, Kaze aliwapa Yanga taji la Mapinduzi baada ya kushinda kwenye fainali mbele ya Simba.

Sasa benchi la ufundi la Yanga litakuwa na Kaze pamoja na Nabi kuelekea kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Septemba 25, Uwanja wa Mkapa watakapomenyana na Simba katika Ngao ya Jamii.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Dominick Albinius amesema kuwa watatoa majibu leo kuhusu kumpa mkataba.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO DIARRA NA JOB WALIVYOIPAISHA YANGA CAF...MSTAA WA SIMBA MHHH...