Home news KIM POLSEN ACHEKELEA KUONGOZA KUNDI, HESABU KUBWA KWA MKAPA

KIM POLSEN ACHEKELEA KUONGOZA KUNDI, HESABU KUBWA KWA MKAPA


 KOCHA  Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen ameridhishwa na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar katika Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa kundi J wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Qatar 2022.

 

Poulsen amesema kuwa ni mafanikio makubwa kwa nchi kuongoza kundi baada ya mechi mbili kwakuwa ni jambo ambalo halijawahi kutokea nchini.

 

“Sote tumeshudia goli la mapema sana dhidi ya Madagascar lakini baada ya kupata bao la pili tumeona wachezaji wangu wakipoteza umakini kitu ambacho kiliwafanya wachezaji wa timu pinzani kurudi mchezoni na kufanikiwa kushinda magoli mawili mpaka muda wa mapumziko.

 

”Tukiwa kwenye vyumba vya kubadilisha nguo sikuwa na budi na kuwambia wachezaji wangu kuwa waache kufanya makosa kwasababu tutaadhibiwa iwapo tutaendelea kupoteza mipira hasa katika eneo letu la hatari, nafurahia kuwa waliitikia wito wangu na baadaye kipindi cha pili tukapata bao la kuongoza na kutengeneza nafasi nyingi zaidi.

 

”Natamani huu Uwanja wa Benjamin Mkapa, uwe uwanja ambao tutashinda mechi zetu zote za nyumbani nikituamia kuwa ni kitu ambacho tutaendelea kukipambania.

 

Pia kocha mkuu ameeleza masikitiko yake baada ya kumkosa John Bocco kwa sababu amekuwa na wakati mgumu wa kuchagua wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji kwa sababu timu nyingi za Tanzania zinasajili wachezaji wakigeni, huku akionesha furaha yake juu ya Reliant Lusajo kwa kuonesha kiwango kizuri kwenye mechi akihudumu katika nafasi hiyo.

 

Baada ya ushindi huo Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Tamaduni na Michezo chini ya Waziri mwenye dhamana, Innocent Bashungwa, amesema kuwa kikosi cha Taifa Stars kitapokea kitita cha Tshs. Million 10 kama motisha kwa kwachezaji.

 

” Kwa matarajio yangu, kwasababu tumejizatiti wakiwa kambini wafanye mazoezi vizuri wakiwa na walimu wazuri pia natoa wito kwa benchi la ufundi kuendelea na moyo huo huo, na kwafuraha niliyonayo kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, tutawaandalia Tshs. Million 10. kama sehemu ya motisha.”

SOMA NA HII  SHABIKI SIMBA:- MGUNDA HANA LOLOTE LILE....HAJAFANYA LA MAANA TOKA APEWE TIMU...

 

Kwa upande wa mchezaji wa Taifa Stars Saimon Msuva amesema kuwa mashindano ni magumu na kila timu imejizatiti kufanya vizuri na zenye wa wachezaji wanaocheza ligi za Ulaya, akisisitiza kuwa timu itakayojipanga vizuri ndiyo yenye nafasi ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.