Home Uncategorized TSHABALALA YEYE MABAO YAKE NI MBELE YA WAKATA MIWA TU, SIRI YAKE...

TSHABALALA YEYE MABAO YAKE NI MBELE YA WAKATA MIWA TU, SIRI YAKE HII HAPA


MOHAMED Hussein, ‘Tshabalala’ nahodha msaidizi wa Simba ni miongoni mwa mabeki wenye urafiki na nyavu na mabao yake yote amezitungua timu za makampuni ya miwa.

Bao lake la kwanza alifunga mbele ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Kagera wakati Simba ikishinda mabao 3-0 na bao lake la pili alifunga mbele ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikishinda mabao 3-0 Uwanja wa Jamhuri, Moro.

Simba ikiwa imefunga mabao 63 amehusika kwenye mabao 4 ambapo amefunga mabao mawili na kutoa asisti mbili za mabao.

Tshabalala amesema:”Kikubwa ni sapoti ya wachezaji wenzangu pamoja na kujituma,” .

Ligi Kuu Bara kwa sasa imesimamishwa na Serikali tangu Machi 17 kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

SOMA NA HII  HERSI ASHINDWA KUFAFANUA JAMBO HILI LA UBINGWA WA YANGA