Home Azam FC MASTAA AZAM KULAMBA MIL 100 WAKIMBATUA YANGA LEO…

MASTAA AZAM KULAMBA MIL 100 WAKIMBATUA YANGA LEO…

Azam FC

Wachezaji wa Azam FC wametengewa Shingili Milion 100 na Uongozi wa Klabu hiyo endapo watafanikisha kutwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya mabingwa watetezi Young Africans kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baadae leo Jumatatu (Juni 12).

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Azam FC kimeeleza kuwa wachezaji watapewa fedha hizo huku wakiahidiwa tofauti na za benchi la ufundi hivyo kazi imebaki kwao kutimiza lengo.

“Viongozi wameweka kiasi hicho ingawa wameahidiwa kuna uwezekano zikaongezeka, hivyo hizo ni za awali tu, ASFC ndilo taji pekee lililobaki kwetu na hatutaki kulipoteza,” kimeeleza chanzo hicho.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema hakuna asiyejua umuhimu wa mchezo huo na wao viongozi tayari wameshatimiza wajibu kwa wachezaji wa timu hiyo.

“Kila mchezaji anajua ahadi ambayo sisi kama viongozi tumeiweka lakini siwezi kusema ni kiasi gani, jukumu limebaki kwao kuhakikisha taji hili wanalipigania ili kumaliza msimu kwa heshima.”

Azam FC ilitinga fainali hiyo baada ya kuifunga Simba mabao 2-1 wakati Young Africans ikiitoa Singida Big Stars kwa bao 1-0 la mtokea benchi, Fiston Kalala Mayele.

SOMA NA HII  GAMONDI ATOA ONYO KUHUSU UBINAFSI KISA MASTAA HAWA