Home Habari za michezo BAADA YA OKRAH….MASTAA WENGINE WANAOTEMWA SIMBA KUJULIKANA LEO….MBRAZILI ASEPA…

BAADA YA OKRAH….MASTAA WENGINE WANAOTEMWA SIMBA KUJULIKANA LEO….MBRAZILI ASEPA…

Habari za SImba SC

KOCHA mkuu wa Simba,Roberto Oliviera (Robertinho) ameondoka juzi usiku kuelekea kwao kwa ajili ya mapimziko ya msimu baada ya msimu wa Ligi Kuu Bara kufikia tamani lakini amewaachia majina ya wachezaji ambao hawatakuwwpo nao msimu ujao ambao leo Simba itayaweka wazi.

Kocha huyo ameondoka na kutoa maagizo mazito ikiwemo ripoti yake usajili ambayo juzi jioni bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo ilikaa kuijadiri kwa mara ya mwisho ikiwemo kupitisha bajeti yake ya usajili mapema.

Inafahamika kuwa Mbrazil huyo amewataka mabosi wa timu hiyo unakini katika orodha ya wachezaji ambao anahitaji kuwa nao katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa ambayo timu itashiriki.

Akizungumza jana, Meneja wa mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally, alisema Mbrazil huyo ameondoka nchini jana (juzi) kuelekea kwao kwa mapumziko huku akiwaachia majina ya wachezaji ambao hawahitaji kwenye kikosi chake cha msimu ujao.

” Ni kweli mwalimu amerejea kwao kwa ajili y mapumziko lakini uongozi kwa sasa unajipanga kuanza kushusha vitu kwa ajili ya msimu ujao na hii imetokana na kushindwa kufanya vizuri katika michuano yote ambayo tumeshiriki msimu huu.

” Kikubwa ni kwamba ametuachia ripoti yake na nini ambacho anahitaji kwa ajili ya msimu ujao na kesho Jumatatu (leo) tunatarajia kuweza wazi kwa kuwatangaza nyota ambao tumewapa mkono wa kweli msimu huu,” alisema Ahmed.

Aliongeza kuwa katika kikao hicho kilichofanyia kwa muda wa siku saba kimefikia tamati jana

Kwa ajili ya kutathimini msimu wa ligi ulimalizika juma lililopit pamoja na kujadili mipango madhubuti kwa msimu ujao wa 2023/24.

Alisema kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti Salim Abdallah ‘Try Again ‘, na wajumbe wote wamehudhuri, Miongoni mwa vitu vilivyojadiliwa ni pamoja na bajeti ambayo kuendelea msimu mpya wa ligi na mshindano yaliyopo mbele yao ikiwemo Super League.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE