Home Habari za michezo STRAIKA WA MABAO ATUA SIMBA….MUDA WOWOTE ATATAMBULISHWA KAMA STAA MPYA MSIMBAZI..

STRAIKA WA MABAO ATUA SIMBA….MUDA WOWOTE ATATAMBULISHWA KAMA STAA MPYA MSIMBAZI..

Tetesi za usajili Simba

SIMBA ipo kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilisha usajili wa mfungaji bora wa Ligi Kuu Rwanda, Leandre Essomba Willy Onana, Mwanaspoti linafahamu.

Straika huyo wa Rayon Sports tayari ameshatua Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha dili hilo la kuja kuichezea miamba hiyo ya Msimbazi kwa msimu wa 2023-2024.

Kinara huyo wa mabao kwa msimu wa 2022-23, alitikisa nyavu mara 16 kwenye ligi na kinachoelezwa tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya jana Jumapili na asubuhi ya leo Jumatatu anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kukipiga kwa Wekundu hao wa Msimbazi.

Mcamerooni huyo alitua Kigali Septemba 2021 kama sehemu ya takriban wachezaji 50 walioenda Rayon Sports kwa majaribio katika dirisha hilo la uhamisho.

Kabla ya kwenda Rayon Sports kwa majaribio, Essomba alijizolea umaarufu mkubwa nchini kwao akiwa na klabu ya Ending Sport FC, inayojulikana huko Cameroon kwa kukuza vipaji vya vijana.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Rayon, fowadi huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga mabao 10 ya ligi lakini kiwango chake kizuri katika msimu wa 2022/23 kilishuhudia idadi ya mabao yake ikiimarika, akifunga mara 16 kwenye ligi na mabao manane kwenye Kombe la Amani.

SOMA NA HII  SIMBA YACHAPWA FAINI NA BODI YA LIGI KISA HIKI HAPA